Tamasha la Kizimkazi ni fursa kubwa ya kiuchumi-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema tamasha la kila mwaka la utamaduni wa watu wa Mkoa wa Kusini Unguja (Kizimkazi Festival) ni fursa kubwa kwa wafanyabiasha na utalii wa visiwa hivyo.
Akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa tamasha hilo leo Agosti 18, 2024 katika Viwanja vya Kizimkazi Dimbani, Dkt. Mwinyi amesema tamasha hilo limewavutia watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi na hiyo ni fursa kwa utalii na biashara kwa Wazanzibar.

Amesema,kumekuwa na ongezeko kubwa la watalii na wananchi wa kawaida wakati wa tamasha hilo, hali inayotoa fursa kwa wafanyabiashara kuonesha biashara zao na kufanya biashara vilevile.

“Nimeambiwa hapa kuwa hoteli zote za Kusini Unguja zimejaa, hii ni ishara kuwa mwitikio wa watalii kuja huku wakati huu wa tamasha ni mkubwa.

"Hii ni fursa kwenu kupanua wigo wa kuwapokea wageni na watalii ili muweze kunufaika na tamaha la Kizimkazi."

Aidha,Dkt.Mwinyi amesema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kumaliza changamoto zinazoukabili Mkoa wa Kusini ikiwa ni pamoja na uhaba wa wafanyakazi sekta ya afya kabla ya kufikia mwaka 2025.

Dkt. Mwinyi amefafanua kuwa, mbali na kuimarisha utalii wa ndani, tamasha hilo linaleta umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi pamoja na kuimarika kwa mila, desturi, na maadili ya Kizanzibari.

Tamasha hilo litaendelea kwa matukio mbalimbali hadi Agosti 25, 2024 ambapo litafungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Tamasha la Kizimkazi awali lilijulikana kama 'Samia Day' na liliasisiwa mwaka 2016 na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuwakutanisha wakazi wa Mkoa wa Kusini Unguja ili kujadili maendeleo ya mkoa wa wao na tangu mwaka 2020 likabadilishwa jina na kuwa Tamasha la Kizimkazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news