NA JONAS KAMALEKI
TANZANIA inajitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya asilimia 120 na hivyo kuwa na uwezo wa kuuza chakula nje ya nchi.
Hii imetokana na Serikali kuwa na mipango madhubuti na kutekeleza mikakati ya kilimo cha kisasa hasa matumizi ya mbolea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi, wakulima, wafanyabiashara, wageni kutoka nchi mbalimbali pamoja na Wananchi wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane.
Hayo yamebainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma leo tarehe 8/8/2024 katika kilele cha Siku ya Wakulima Nanenane.
Kilimo hapa Tanzania kinaendelea kupewa kipaumbele kwa kutengewa bajeti kubwa ambayo itatekeleza miradi mbalimbali ya umwagiliaji. Bajeti ya kilimo imetoka kwenye shilingi bilioni 294 hadi trilioni 1.248.
"Nawashukuru sana wakulima kwa kazi kubwa mnazozifanya za kulilisha Taifa,"alisema Rais Dkt. Samia.
Aidha, Dkt. Samia amesema kuwa bajeti ya mifugo imeongezwa kutoka shilingi bikini 60 hadi. zaidi ya bilioni 200.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasha moja ya trekta la kisasa mara baada ya hafla ya makabidhiano ya zana za kilimo kwenye kilele cha Siku Kuu ya Wakulima katika viwanja vya Maonesho hayo, Nzuguni Jijini Dodoma tarehe 08 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mfano wa Ufunguo Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe kama ishara ya makabidhiano ya Zana za mbalimbali za Kilimo Matrekta 519, Power Tiller 800, Majembe ya kulimia 200 wakati wa kilele cha Maonesho ya Nanenane.
Rais Samia amegawa matrekta 600 kwa wakulima na kuzindua kiwanda cha kuunganisha matrekta. Hii itapunguza gharama za kununua matrekta hayo.
Aidha, Rais Samia amesema ifikapo mwaka 2030 Serikali itakuwa imepeleka matrekta elfu 10 na power tiller elfu 10 kwa wakulima.
Katika kuhakikisha mazao yanahifadhiwa vizuri, Serikali imejenga maghala makubwa na ya kisasa katika mikoa mbalimbali nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa mbalimbali za kilimo zilizotokana na bustani zilizopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma tarehe 08 Agosti, 2024.
Maonesho ya Nanenane mwaka huu yamefanyika Kitaifa Dodoma baada ya kuzinduliwa tarehe 1/8/2024 na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa leo tarehe 8/8/ 2024 na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.