Tanzania yamuunga mkono Raila Odinga kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa AU

NAIROBI-"Tanzania inamuunga mkono Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amolo Odinga katika kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU). 

"Watanzania wanamfahamu Mheshimiwa Odinga kama mwanamajumui wa Afrika anayeamini katika mtangamano wa Afrika na manufaa yake.

Binafsi, nakupongeza Mheshimiwa Odinga kwa kudumisha mahusiano mazuri na Viongozi wa Afrika na wabia wake. 

"Tunaamini kuwa wewe ni kiongozi mwenye busara na mwenye uwezo wa kujenga Umoja wa Afrika thabiti, unaochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya bara la Afrika na wenye uwezo wa kutetea maslahi ya Afrika kimataifa.Tunakutakia kila la kheri,"amesisitiza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Agosti 27,2024.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye hafla ya uzinduzi wa kapeni ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Raila Amolo Odinga anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto.
kutokakushoto ni Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Raila Amolo Odinga akizungumza wakati wa hafka ya uzinduzi wa Kampeni ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika( AU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news