MARA-Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi, ametoa pongezi kwa Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwa kuendesha kampeni ya "Kilimo ni Mbolea" yenye kauli mbiu "Ongeza Mavuno kwa Matumizi Sahihi ya Mbolea" iliyofanyika katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa Mashariki, hususan Simiyu na Mara.

Ameongeza kuwa, matumizi ya mbolea katika mikoa hiyo bado yako chini ya asilimia 40, hivyo ameahidi kuwa Serikali za Mikoa husika zitafanya jitihada kuhakikisha wakulima wanajitokeza kusajiliwa ili kunufaika na mbolea za ruzuku zinazotolewa na serikali ya Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu hassan.
Pia, amewasihi wananchi kujitokeza kuhuisha taarifa zao kwenye daftari la wapiga kura na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024.
