ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea nchi dua na viongozi wake waendelee kudumisha amani, mshikamano utulivu kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Agosti 2,2024 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa Msikiti wa Rahman Taveta, Mkoa wa Mjini Magharibi.