Tujitokeze kwa wingi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa-DED Asia Messos

SINGIDA-Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Asia Messos amewataka wananchi wilayani Mkalama kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba, 2024.
Wito huo ameutoa Agosti 26,2024 wakati wa ziara ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa vijiji vya Gumanga na Nduguti wilayani hapa

“Nawasihi msipoteze haki zenu za msingi, utakapofika wakati wa kujiandikisha, mjiandikishe, utakapofika wakati wa kampeni jitokeze na itakapofika wakati wa kupiga kura Novemba 27, 2024 tujitokeze kuwachagua viongozi wetu tunaowataka,” Bi. Asia Messos.

Akizungumzia suala la maadili, Bi.Asia Messos amewakumbusha wakazi wa vijiji vya Nduguti na Gumanga kuwa mstari wa mbele kupinga mila na desturi zinachochea mmomonyoko wa maadili katika jamii.
“Tujikite sana katika malezi yetu, turudi katika misingi yetu ya kitanzania. Hii iwe ajenda kubwa katika mikutano yetu, katika nyumba zetu za ibaada. Tuungane pamoja kupinga ushoga na usagaji katika jamii zetu” Bi. Asia Messos.

Aidha,Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Mkalama amewataka wazazi wilayani hapa kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule kwa manufaa ya maisha ya baadae pamoja na kusisitiza suala la kuchangia chakula shuleni.

Awali akielezea mambo makubwa yaliyofanywa na serikali katika miaka 3 ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bi. Asia Messos amesema Halmashuri ya wilaya ya Mkalama imepokea zaidi ya bilioni 60 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya elimu,afya umeme,Barabara pamoja na kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news