Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania yatoa wito kwa Watanzania

DODOMA-Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imewasisitiza Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni mbalimbali kuhusu sheria ambazo wanaona zinamapungufu na zinahitaji marekebisho ili tume hiyo iweze kuzipitia na kuzifanyia tafiti kwa ajili ya kuzirekebisha kabla ya mapendekezo hayo kupelekwa serikalini.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania George Mandepo akiingia kwenye banda la Tume hiyo lililopo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Nane nane yanayofanyika kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Kauli hiyo imetolewa Agosti 6,2024 na Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania George Mandepo,mara baada ya kutembelea banda la Tume hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Mandego amesema, wajibu mkubwa wa Tume hiyo ni kupendekeza marekebisho ya sheria, kufutwa kwa sheria au kuboresha mifumo ya usimamizi wa sheria ambazo zipo Serikalini ili ziweze kutenda haki kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania George Mandepo akisaini Kitabu cha Wageni.

“Tume kabla ya kurekebisha sheria inafanya utafiti kwa uhakika kuhusu sheria husika kwa kuangalia mazingira ya sasa na mazingira yajayo kwa sababu sheria inaishi”, Amesisitiza Mandego.

Katibu Mtendaji huyo wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania amesema pamoja na Tume kufanya mapitio ya sheria na kuzirekebisha pia ina wajibu wa kuangalia iwapo sheria inayotungwa kama inaweza inaweza kuleta madhara ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.Maafisa wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakimpatia maelezo kuhusu namna ya kazi ya kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda hiyo inavyofanyika.

Ameeleza kuwa, mchakato mzima kwa kurekebisha sheria inashirikisha kikamilifu wadau wa sekta husika ikiwemo wananchi ili kuhakikisha sheria inayotungwa inakuwa bora kwa ajili ya maslahi ya mapana ya pande zote Mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news