Tumedhamiria kuifungua Pemba kiuchumi-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Serikali imeazimia kuifungua Pemba kiuchumi kwa kutekeleza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba, barabara za kutoka Chake hadi Mkoani, Chake hadi Wete, pamoja na bandari za Wete, Shumba Mjini na Mkoani.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Agosti 21, 2024, alipozungumza na Wajumbe wa Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu ya CCM ngazi ya Tawi, Wadi, Majimbo, Wilaya, na Mkoa katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha, Dkt. Mwinyi amewahimiza wanachama wa CCM kuhubiri amani, umoja, na mshikamano. 

Pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Kupiga Kura mwakani.

Rais,Dkt. Mwinyi amesema kuwa ametekeleza vema Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 kwa kuvuka malengo ya ilani hiyo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, barabara, masoko, na kadhalika.

Halikadhalika, Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa CCM itashinda kwa kishindo mwaka 2025 kwa sababu imetekeleza vema ilani na kuvuka malengo waliyoyaahidi kwa wananchi.

Vilevile, Dkt. Mwinyi amesema kuwa katika awamu mpya ya mwaka 2025-2030, kasi ya maendeleo ya Zanzibar itakuwa ya hali ya juu.

Kwa upande mwingine, Dkt. Mwinyi amesema kuwa Serikali itamaliza changamoto za miradi ya umeme na maji katika kipindi kilichobaki, pamoja na kutekeleza ahadi zote zilizoahidiwa wakati wa kampeni za mwaka 2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news