Ubaya Ubwela, Simba SC yaichapa Fountain Gate FC mabao 4-0

NA DIRAMAKINI

SIMBA SC ya jijini Dar es Salaam imejizolea alama tatu zikisindikizwa na mabao 4'0 baada ya kutembeza kichapo kwa Fountain Gate FC.

Ni kupitia mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao umepigwa leo Agosti 25,2024 katika dimba la KMC Complex lililopo Mwenge katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Edwin Balua awapatia Simba SC bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 13, baada ya kumalizia mpira krosi uliopigwa na Jean Charles Ahoua.

Aidha, Steven Mukwala aliwapatia bao la pili dakika ya 44 baada ya kumalizia pasi safi kutoka Shomari Kapombe.

Naye Jean Ahoua aliwapatia bao la tatu dakika ya 59 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka Balua.

Valentino Mashaka aliwapatia bao la nne dakika ya 81 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Ahoua.

Ushindi huo unawafanya Simba SC kufikisha alama sita baada ya kucheza mechi mbili wakifunga mabao saba huku wakiwa hawajaruhusu bao lolote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news