Ujenzi wa Mahakama tatu za mwanzo Rukwa waiva

NA MAYANGA SOMEKE
Mahakama

UJENZI wa Mahakama za Mwanzo tatu katika Mkoa wa Rukwa utaanza hivi karibuni baada ya Mahakama ya Tanzania kukabidhi maeneo ya miradi hiyo kwa Mkandarasi, Bw. Nassir Mohamed kutoka kapuni ya Skywards Co. LTD.
Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga, Bw. Machumu Essaba na Mshauri Elekezi kutoka Kampuni ya Norplan(T) LTD, Bw. Elton Maro akimkabidhi nyaraka za kiwanja cha Kasanga, Wilaya ya Kalambo Mkandarasi, Bw. Nassir Mohamed kutoka Kampuni ya Skywards Co. LTD.

Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga, Bw. Machumu Essaba alikabidhi maeneo hayo kwa niaba ya Mahakama ya Tanzania, tukio ambalo lilishuhudiwa na Wawakilishi kutoka Makao Makuu ya Mahakama na Viongozi wengine.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Bw. Essaba alimhimiza Mkandarasi huyo na Mshauri Mwelekezi, kutekeleza makubaliano ya mkataba wa ujenzi wa Mahakama hizo Nambogo, Kasanga na Namanyere ili ziweze kukamilika kwa wakati.
Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Sumbawang,a Bw. Machumu Essaba akiwa Pamoja na wageni katika ofisi yake.

Mahakama ya Mwanzo Nambogo itajengwa katika Wilaya ya Sumbawanga, Mahakama ya Mwanzo Kasanga itajengwa katika Wilaya ya Kalambo na Mahakama ya Mwanzo Namanyere itajengwa katika Wilaya ya Nkasi.

Mtendaji huyo alieleza kuwa Wakandarasi Wazawa wamekuwa wakipokelewa vizuri baada ya kuaminiwa na kupelekwa kwenye miradi kwa ajili ya utekelezaji wa mikataba, lakini wamekuwa wakishindwa kwenda na mpango kazi waliowasilisha wao wenyewe, badala yake huleta visingizio endelevu na kuchelewesha ujenzi.
Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Sumbawang,a Bw. Machumu Essaba na Mshauri Elekezi kutoka Kampuni ya Norplan(T) LTD, Bw. Elton Maro wakimkabidhi nyaraka za kiwanja cha Nambogo, Wilaya ya Sumbawanga Mkandarasi, Bw. Nassir Mohamed kutoka Kampuni ya Skywards Co. LTD.

“Hali hii hatutaivumilia wala hatutaikubali kwa muda wote tutakaosimamia miradi, pasiwepo na neno changamoto kwenye majadiliano yetu yote mpaka kukamilisha kwa miradi,”alisema.

Alieleza kuwa hawatasita kumjulisha Mshauri msimamizi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama kwa maandishi kufuta mara moja kandarasi hiyo kwenye mkoa wa Rukwa kama wataona dalili za kusuasua kwa mradi na viashiria vyovyote vya kwenda nje na mpango kazi.
Mtendaji wa Mahakama Kuu kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu Essaba na Mshauri Elekezi kutoka Kampuni ya Norplan(T) LTD, Bw. Elton Maro akimkabidhi nyaraka za kiwanja cha Namanyere, Wilaya ya Nkasi Mkandarasi, Bw. Nassir Mohamed kutoka Kampuni ya Skywards Co. LTD.

Naye Mshauri wa Majengo(Consultancy) kutoka Kampuni ya NORPLAN(T) LTD, Bw.Elton Maroalisema miradi yote mitatu itakwenda kwa pamoja na itadumu ndani ya miezi sita kuanzia tarehe 12 Agosti, 2024.

Bw.Maro alisema kwamba, Mkandarasi huyo amepewa siku 14 ya kufanya maandalizi ya vifaa vya ujenzi pamoja rasilimali watu na atatakiwa kukamisha mradi mwezi Februari, 2025 na kukabidhi Mahakama hizo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za haki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news