VIDEO:Gavana Tutuba,uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika

NA DIRAMAKINI

"Kwa Tanzania kwa kweli kwanza tunashukuru kwamba katika Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama yetu Dkt.Samia Suluhu Hassan suala zima la uchumi umeendelea kuwa imara. Ndiyo maana utaona mashirika kama ya IMF,World Bank wameendelea kuisifia Tanzania kwa sababu tunafanya vizuri zaidi na hata ukisoma kwenye taarifa zilizotolewa majuzi za credit ratings kwa Moody's na Fitch wote wameendelea kuonesha kwamba,Tanzania tumesimamia suala la uchumi vizuri zaidi.
"Ndiyo maana pale kwenye suala kama la mfumuko wa bei utaona kwamba mfumuko wa bei wa Tanzania upo kwenye kiwango cha asilimia kama 3 mpaka 3.2 kwa kipindi cha miezi sita sasa na hii ni kwa sababu tunavyosimamia suala la mfumuko wa bei, sisi kama Benki Kuu siku zote tunakuwa tuna-regulate kiwango cha fedha kinachoingia kwenye mzunguko.

"Ili kupata thamani ambayo unaweza ukaendelea kufanya miamala,kwa hiyo ukiangalia suala la ujazi wa fedha kwenye uchumi kwa sasa linaendana na shughuli zilizopo kwenye mzunguko,"amesisitiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Emmanuel Tutuba katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane yaliyofanyika Kitaifa viwanja vya Nzunguni jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news