Viongozi wapya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wapokelewa Dar

DAR-Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Johari akiambatana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Samwel Maneno, leo Agosti 15,2024 wametembelea na kupokelewa katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilizoko Kivukoni jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wamefika kwenye Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam, na kupokelewa na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Balozi Prof. Kennedy Gastorn, Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Akizungumza katika hafla fupi ya ukaribisho Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Johari, aliwashukuru aliekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Menejimenti ya Watumushi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mapokezi mazuri aliyoyapata kwenye Ofisi hiyo.

“Nianze kwa kuwashukuru sana kwa mapokezi mazuri niliyoyapata kwani taarifa imetoka ndani ya muda mchache lakini mmeweza kutuandalia shughuli hii fupi ya mapokezi, nawapongeza na kuwashukuru sana na nawaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha."
Kwa upande wake aliekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, amewakaribisha na kuwapongeza Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuteuliwa kushika nyadhifa hizo, huku akiwaahidi kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Niwapongeze sana kwa kupata uteuzi huu, mimi binafsi nawaahidi kuwapa ushirikiano wa mkubwa, leo tumewakaribisha tu muijue ofisi hii ya Dar es Salaam, muda si mrefu tutakutana tena kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya nyaraka mbalimbali za kiofisi.”
Baada ya hafla hiyo ya ukaribisho, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Hamza Johari pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Samwel Maneno wanatarajia kukutana na Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu waliopo Jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news