Vyama vya siasa msiingilie mchakato wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura-Jaji Mwambegele

MARA-Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeviasa vyama vya siasa kutoingilia mchakato wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika vituo vya kuandikishia wapiga kura.
Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara. Wadau hao ni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.

Wito huo umetolewa leo tarehe 25 Agosti, 2024 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jacobs Mwambegele, wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika mkoani Mara.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara. Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara. Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.

Mhe. Jaji Mwambegele amesema mawakala au viongozi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi kuingilia mchakato wa uboreshaji vituoni kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria ya uchaguzi.

Amehimiza viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia sheria ya uchaguzi, kanuni za uboreshaji, maelekezo ya tume, na kusimamia miiko na mipaka ya uendeshaji wa zoezi la uboreshaji wa Daftari.

Pia amevitaka vyama vya siasa kutumia sheria zilizopo kuwasilisha changamoto zinazojitokeza kwa tume, ambapo ameongeza kuwa INEC itazingatia Katiba, sheria ya uchaguzi, na kanuni zilizotungwa chini ya sheria katika zoezi la uboreshaji.
Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akiongoza majadiliano.

Aidha, Jaji Mwambekele alieleza kuwa zoezi lililofanyika Novemba, 2023 Katika Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, mkoani Mara lilikuwa la majaribio.

Hivyo, wananchi wote wa Kata ya Ikoma ambao walijitokeza kwenye zoezi husika, wanapaswa kujitokeza kwenye uboreshaji utakaoanza rasmi tarehe 04 hadi 10 Septemba, 2024 ili taarifa zao ziweze kuhifadhiwa rasmi kwenye mfumo wa Daftari.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Bw. Kailima Ramadhani akijibu hoja mbalimbali wakati wa mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara.

Akiwasilisha mada kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhan Kailima amsema, tume inategemea vyama vyenye usajili kamili kutumia fursa za kisheria zilizotolewa kwao kuhakikisha zoezi la uboreshaji linafanikiwa na kuongeza kuwa endapo kutajitokeza changamoto zozote wakati wa zoezi, Vyama vitumie taratibu zilizoainishwa kwenye sheria kuwasilisha changamoto hizo.
Wadau wakishiriki katika majadiliano.
Wadau wa uchaguzi wakiwa katika majadiliano.

“Viongozi wa vyama hawapaswi kuingilia utekelezaji wa majukumu ya watendaji wa vituo wakati wote wa uandikishaji wa wapiga kura vituoni kama kuomba orodha au idadi ya walioandikishwa au kuboresha au kuhamisha taarifa zao.”
Mkurugenzi wa Daftari na TEHAMA wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Stanslaus Mwita akiwasilisha mada ya mifumo wakati wa mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara.

Ameeleza kuwa, Tume inaowajibu wa kuwapatia vyama vya siasa taarifa hizo mara baada ya zoezi kukamilika.

Mkutano kama huo umefanyika pia mkoani Simiyu na Manyara ambapo akifungua mkutano mjini Bariadi, mkoani Simiyu, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk S. Mbarouk, amewataka wadau kuwaelimisha wananchi kujiandikisha mara moja tu ili kuepuka uvunjaji wa sheria.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akizungumza wakati akiwasisha mada ya maandalizi ya uboreshaji kwa wadau wa uchaguzi Mkoa wa Mara.

Naye Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari, ambaye alifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Manyara, amewahimiza watu wenye ulemavu, wazee, wagonjwa, wajawazito, na akina mama wenye watoto wachanga watakaokwenda nao vituoni kujitokeza kwa wingi kwa kuwa watapewa fursa ya kuhudumiwa bila kupanga foleni.
Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Bw. Kailima Ramadhani wakati wa mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara.

Mikutano hiyo ni maandalizi ya mzunguko wa nne wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha mkoa wa Mara, Simiyu na baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Manyara ambazo ni Halmashauri ya Mji wa Babati na Halmashauri za Wilaya za Babati, Hanang na Mbulu ambapo uboreshaji utaanza tarehe 04 Septemba, 2024 hadi 10 Septemba, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news