Waazimia muda ukifika kumchukulia Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete fomu

PWANI-Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kiwangwa iliyopo Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, wameahidi kumchukulia fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge, Mbunge wao Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Kauli ya wanachama hao ilitolewa mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho ngazi ya kata, ulioandaliwa na Diwani Malota Kwaga ambapo alisema kuwa,azimio hilo limetolewa katika moja ya vikao vya chama hicho.

Mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana Ajira na wenye Ulemavu,Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa jimbo hilo, Kwaga alisema kuwa hatua hiyo inatokana na kazi kubwa inayoendelea kutekelezwa na mbunge wao ndani ya Kata na jimbo kwa ujumla.

"Mheshimiwa Waziri tunamshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu kwa kazi kubwa ya kuwatumikia waTanzania pia kuonesha imani kwako, nasisi tunakupongeza kwa namna unavyodhihirisha kuwa ni mchakapakazi," alisema Kwaga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Hassani Mwinyikondo alisema kuwa maendeleo ya Chalinze yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na Ridhiwani, kwani yeye ndio anayechukua changamoto zao kisha kumpelekea Rais Samia.

"Msione vinaelea mjue vimeundwa na muundaji wetu kwa Chalinze ni Ridhiwani Kikwete, kwetu katika nafasi ya ubunge tumefunga mjadala hatutaraji kumuona mwana CCM yeyote atayechukua fomu, mbunge wetu ni Ridhiwani," alisema Mwinyikondo.

Akizungumza na wana CCM hao, Mheshimiwa Ridhiwani alisema kuwa, kuonekana kwake kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kumechangiwa na wana Chalinze waliomchagua kushika nafasi hiyo, na kwamba Rais asingemuona kama asingekuwa Mbunge.

"Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameniona na kuniteua katika nafasi hii kutokana na nyie wana Chalinze kunichagua kuwa Mbunge wenu ndio Rais akaniona, nawahakikishia kwamba nitaendelea kuipeperusha vizuri bendera ya wana Chalinze," alisema Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news