Wadau waitikia wito wa Rais Dkt.Samia wa kuongeza thamani madini nchini

MANYARA-Kampuni ya Permanent Minerals Ltd iliyopo Kijiji cha Kandaskira wilayani Simanjiro inaendelea na ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata madini kinywe, ambacho kitaongeza fursa kubwa ya kiuchumi kwa wananchi wa Wilaya ya Simanjiro.
Akitoa maelezo mafupi,mmoja wa wamiliki wa kiwanda hicho, Godlisten Mwanga amesema, kiwanda hicho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuchakata tani 108,000 kwa mwaka na kitatoa ajira 300 za moja kwa moja huku Halmashauri ya Simanjiro ikitegemewa kuongeza mapato kupitia uwekezaji huo.
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia alielekeza juu ya uongezaji thamani madini nchini,na sasa tunaona wawekezaji na hasa wawekezaji wazawa wameanza kuitikia wito huo.

"Tanzania imebarikiwa kuwa na madini haya ya kinywe katika maeneo mengi nchini ikiwemo hapa Mirerani,Simanjiro.

"Tutaendelea kuongeza nguvu ya utafiti ili kuvutia uwekezaji mkubwa katika eneo hilo ambalo madini maarufu hapa ni Tanzanite, lakini kutokana na uhitaji mkubwa wa madini kinywe duniani ninaamini uwekezaji wa kutosha pia utafanyika katika kuchimba na kuchakata madini haya."
"Tanzania kwa sasa ni ya tatu katika uzalishaji wa madini kinywe katika Bara la Afrika,ikitanguliwa na Madagascar na Msumbiji.

"Tunaamini kwamba leseni 10 zote za kati na kubwa za uchimbaji madini kinywe zikianza kufanya kazi nchi yetu itakuwa miongoni mwa nchi vinara wa uzalishaji madini kinywe Afrika,”amesema Mavunde.

Akitoa salamu,Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amepongeza uwekezaji huo mkubwa wa kiwanda na kuwasilisha kwa kiwanda maombi ya ajira kutoa kipaumbele wanajamii wanaozunguka kiwanda na pia jamii kunufaika na CSR.
Akimkaribisha mgeni rasmi,Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro,Mheshimiwa Fakhi Lulandala amewahakikishia wawekezaji hao ushirikiano kutoka serikalini na kutoa wito kwa wawekezaji wengi zaidi kuwekeza katika wilaya hiyo yenye utajiri wa madini mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news