Wakala na mfanyabiashara ya pikipiki hatiani kwa rushwa

KAGERA-Agosti 27, 2024 Mahakama ya Wilaya ya Bukoba imemhukumu, Bw. Sadati Rweyemamu ambaye ni wakala na mfayabiashara wa kuuza pikipiki Kagera kwa kosa la ukwepaji kodi kwa kutotoa risiti za Mashine za Kielektroniki (EFD) na kupelekea kukwepa kodi ya kiasi cha shilingi 5,949,152.
Adhabu hivyo imetokana na mshtakiwa kushtakiwa kwa Rushwa kinyume na kifungu cga 15 (1) (a), 2 cha PCCA na Kujipatia fedha na manufaa yasiyostahili.

Ni baada ya kuuza pikipiki 10 zenye thamani ya sh. 39,000,000 na kosa la kutotumia risiti ya Efd katika mauzo hayo kinyume na kifungu cha 86 (1), (b) na (3) cha Sheria za Usimamizi wa Kodi Sura ya 438 Marejeo ya 2022.

Hukumu hiyo dhidi ya Sadati Siraji Rweyemamu katika Kesi ya Rushwa namba 15406/2024 imesomwa na Mhe. Andrew Kabuka, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba, mbele ya Wakili wa Jamhuri (PCCB), Kelvin Murusuri.

Mshitakiwa ametiwa hatiani kwa kuamriwa kulipa faini ya sh 3,000,000 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Pia, Mahakama kufuatia maombi ya Wakili Murusuri imemuamuru mshtakiwa kulipa kodi hiyo ya Serikali sh. 5,949,152 ndani ya miezi mitatu.

Mshtakiwa amekwenda Gerezani kungojea taratibu za upatikanaji wa fedha za kulipia faini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news