Wakandarasi Mradi wa TAZA (kV 400) watakiwa kukamilisha kazi kwa wakati

DAR-Leo Agosti 17, 2024 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameongoza kikao cha Tatu cha Kamati ya Uongozi ya Mradi wa usafirishaji umeme wa msongo wa kilovoti 400 wa Tanzania- Zambia (TAZA) kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kilichojadili utekelezaji wa mradi hadi kufikia Julai, 2024, kimewataka wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo kukamilisha kazi mapema kwa mujibu wa mkataba.
Mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa TAZA unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia, ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Iringa, Mbeya, Tunduma na Sumbawanga pamona na mfumo wa kutoa huduma ambao utawezesha kuunganisha Bara la Afrika kwa nishati ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia.
Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na taasisi zake pamoja na Wizara ya Fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news