Wananchi waendelea kujifunza mengi kutoka BoT maonesho ya Nanenane
DODOMA-Wataalamu kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakitoa elimu kuhusu kazi mbalimbali za BoT kwa wananchi wanaotembelea banda letu kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo-Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma.
Miongoni mwa kazi za BoT ambazo wananchi wanapata fursa ya kujifunza ni pamoja na utekelezaji wa sera za fedha, namna ya kuwekeza katika dhamana za serikali, mifumo ya malipo ya taifa, na namna BoT inavyosimamia sekta ya fedha nchini.
Vilevile, BoT inaelimisha umma kuhusu utatuzi wa malalamiko ya mtumiaji wa huduma za fedha, masuala ya ajira na utumishi Benki Kuu, pamoja na nafasi za masomo katika Chuo cha BoT.
Pia, Benki Kuu inatoa elimu kuhusu utambuzi wa alama za usalama katika noti za Tanzania na njia sahihi za utunzaji wa noti na sarafu. Wananchi wanaotembelea banda la BoT wanapata fursa ya kuona na kujifunza kwa vitendo alama hizi muhimu zinazosaidia kutambua noti halali za Tanzania.