Wananchi wajionea utekelezaji miradi ya gesi asilia Nanenane Dodoma

DODOMA-Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yamekuwa ni sehemu ya wananchi kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Sekta ya Nishati ikiwemo miradi ya Gesi Asilia na Mafuta.
Katika Banda la Wizara ya Nishati wananchi wameonesha kuvutiwa na teknolojia ya Uhalisia.
Pepe (Virtual reality) ambayo inawawezesha wananchi kuona moja kwa moja miradi ya uzalishaji, uchakataji na usambazaji wa gesi asilia iliyopo mkoani Mtwara na Lindi.

Kupitia teknolojia hiyo wananchi wameweza kuona namna gesi inavyozalishwa kutoka kwenye visima na kuingiwa kwenye mitambo ya uchakataji kisha kusafirishwa kwa bomba kwenda kwenye matumizi mbalimbali ya viwandani, kuzalisha umeme, kwenye magari, taasisi pamoja na matumizi ya majumbani.

Aidha, Wizara ya Nishati inaendelea kutoa elimu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news