Wanufaika batili wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wafikishwa mahakamani Dar

DAR-Shauri la Uhujumu Uchumi Namba 23263/2024 lilifunguliwa Agosti 19, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Ilala mkoani Dar es Salaam mbele ya Mheshimiwa Battony Mwakisu ambaye ni Hakimu Mkazi Mwandamizi.
Shauri hilo linahusisha washtakiwa watatu akiwemo;

1.Flora Robert Urio ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Gerezani katika Halmashauri ya Manispaa Ilala mkoani Dar es Salaam.

2.Fidelis Casmir Shirima ambaye ni mjasiriamali na;

3.Edinister Issack Minja aliyekuwa Afisa Mikopo kampuni binafsi ya PTF).

Wote walishtakiwa kutenda jumla ya makosa tisa yakiwemo; kughushi, kuwasilisha nyaraka zenye maelezo ya uongo kwa nia ya kumdanganya mwajiri.

Vile vile,kula njama na kuisababishia Serikali hasara ya kiasi cha shilingi milini 53.23.

Washtakiwa Fidelis Shirima na Edinister Minja walikiri kutenda makosa hayo ambapo Mahakama iliwatia hatiani na kuhukumiwa kifungo cha nje kwa muda wa mwaka mmoja.

Aidha, walitakiwa kurejesha kiasi cha shilingi milioni 18 kila mmoja ndani ya mwaka mmoja tangu kutolewa kwa hukumu.

Mshtakiwa Flora Urio alikana kutenda makosa hayo na shauri limepangwa kusikiliza hoja za awali Agosti 25,2024 na yuko nje kwa dhamana.

Shauri hilo lilitokana na uchunguzi wa tuhuma ya kughushi na kutumia Cheti cha Ndoa inayodaiwa kufungwa baina ya Bi. Flora Urio na Bw. Fidelis Shirima na hivyo kumwezesha Bw. Shirima kupata kadi ya mnufaika wa NHIF aliyoitumia kwa vipindi tofauti kupata matibabu mbalimbali na kusababisha NHIF kupata hasara ya shilingi 53,227,555.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news