DODOMA-Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri, amesema Wizara ya Maji imeandaa mafunzo ya siku mbili katika kuhakikisha usalama wa mabwawa ya maji na tope sumu unaimarishwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri.
Amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na TanzaniabChamber of Mines na yatafanyika mkoani Mwanza.
Amesema hayo katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Maji uliopo Mtumba jijini Dodoma.
Ameongeza kuwa, mafunzo yatahusisha watalaam kutoka wamiliki wa migodi kwa ajili ya usalama wa mabwawa ya tope sumu, wamiliki wa mabwawa makubwa ya maji, wataalam wa mabwawa waliosajiliwa na wataalam kutoka Serikalini.
