DAR-Kwa hakika wameshangaa kwa nini hawapo 10 Bora ya nchi zinazoleta watalii kwa wingi na wameshangazwa zaidi na uzuri wa Tanzania; huo ndio mtazamo wa awali kabisa wa kundi la makampuni makubwa ya utalii na vyombo vya habari vya masuala ya safari waliofika nchini leo tayari kuitembelea na kuona uzuri wa Tanzania.


Naye Balozi wa Tanzania nchini Brazil Balozi Profesa Adelardus Kilangi amesema safari hiyo imetokana na ushiriki wa Tanzania wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa WTM ((World Tourism Market) Latin America na moja ya ajenda ilikuwa ni kuitambulisha Tanzania katika soko la utalii la Brazil.
Naye Mratibu wa mawakala hao Bi. Luciana Teixeiana amesema wanafuraha kufika Tanzania na kufurahia mandhari ya jiji zuri la Dar es salaam na wanatumaini watafarijika zaidi na safari yao katika vivutio mbalimbali nchini wakianzia na Serengeti, Ngorongoro na kisha Zanzibar.
Mawakala hao watakuwepo nchini kwa siku 7 na kati yao zipo kampuni mashuhuri za Kibrazil zinazopeleka mamilioni ya watalii nje ya nchi yao ambazo ni kampuni za JACOB Turismo, Golden travel na T4T.