Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watakiwa kutoa ushirikiano kwa tume na wadau

MARA-Watendaji wa uchaguzi katika mikoa ya Mara, Simiyu na Manyara wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na wadau wa uchaguzi wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kufanikisha zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mikoa yao.
Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Agosti 26 hadi 27, 2024 mkoani Mara.

Wito huo umetolewa leo tarehe 26 Agosti, 2024 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele wakati akifungua mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa watendaji wa uboreshaji ngazi ya mkoa na halmashauri yaliyofanyika katika mji wa Musoma mkoani Mara.

Jaji Mwambegele amesisitiza kuwa ni muhimu kwa watendaji hao kuhakikisha kuwa wanafuata maelekezo ya Tume na kushirikiana kikamilifu ili kuhakikisha zoezi la uboreshaji linaenda vizuri na kwa ufanisi.
Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Agosti 26 hadi 27, 2024 Mkoani Mkoani Mara.

“Ninawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa karibu na Tume wakati wote mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu na ikiwa mnahitaji ufafanuzi au maelekezo yoyote, msisite kuwasiliana na Tume,” amesema Jaji Mwambegele.
Makamu Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji wa Rufaa(Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Agosti 26 hadi 27, 2024 Mkoani Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Selemani Mtibora akizungumza wakati wa mafunzo hayo mkoani Simiyu.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Agosti 26 hadi 27, 2024 Mkoani Mkoani Manyara.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giviness Aswile akizungumza jambo wakati wa Mafunzo hayo mkoani Manyara.
Washiriki wa Mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Simiyu, wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao. Mafunzo hayo yameanza leo Agosti 26, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Simiyu.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk ambaye alifungua mafunzo kama hayo mkoani Simiyu amewataka watendaji hao kutoa ushirikiano kwa mawakala wa vyama vya siasa, asasi za kutoa elimu ya mpiga kura na waangalizi wa zoezi hilo.

Mkoani Manyara, mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi ngazi ya mkoa yalifunguliwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari ambaye amewataka watendaji hao kuzingatia mafunzo hayo ili waweze kuwafundisha Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata.

“Mafunzo haya yanawajengea umahiri wa kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata ili nao wakatoe mafunzo hayo kwa waendeshaji wa vifaa vya Bayometriki na Waandishi wasaidizi ambao ndiyo watakaohusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni,” amesisitiza Jaji Asina.
Washiriki wa Mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Manyara, wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao. Mafunzo hayo yameanza leo Agosti 26, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Manyara.
Washiriki wa Mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Manyara, wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao . Mafunzo hayo yameanza leo Agosti 26, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Manyara.

Washiriki wa Mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Mara, wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Musoma,Bi. Aristida Tarimo. Mafunzo hayo yameanza leo Agosti 26, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Mara.
Washiriki wa Mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Mara, wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Musoma,Bi. Aristida Tarimo. Mafunzo hayo yameanza leo Agosti 26, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Mara.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Musoma,Bi. Aristida Tarimo akitoa maelekezo kabla ya kuwaapisha.
Kufanyika kwa mafunzo hayo, ni maandalizi ya kuanza kwa mzunguko wa nne wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao unajumuisha mkoa wa Mara, Simiyu na baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Manyara ambazo ni Halmashauri ya Mji wa Babati na Halmashauri za Wilaya za Babati, Hanang na Mbulu ambapo uboreshaji utaanza tarehe 04 Septemba, 2024 hadi 10 Septemba, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news