Watendaji wa vijiji hatiani kwa tuhuma za ubadhirifu Katavi

KATAVI-Agosti 27, 2024 mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ambaye ni Mtendaji wa Kijiji cha Kamsisi, amefikishwa mahakamani na kufunguliwa shauri namba 24458/2024.
Shauri hili linahusu ubadhirifu na ufujaji kinyume na kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Mshtakiwa huyo katika nyakati tofauti alikuwa akikusanya ushuru wa mazao katika Kijiji cha Kamsisi na kutowasilisha fedha benki kiasi cha shilingi 17,456,300

Shauri tajwa limesomwa mahakamani na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Wakili Kelvin Mwaja mbele ya Mheshimiwa Jackson Ryoba ambaye ni Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Mlele.

Mshtakiwa amekana mashtaka yote na yupo nje kwa dhamana. Kesi hiyo itakuja tena mahakamani Septemba 5,2024 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.

Wakati huo huo, Agosti 27, 2024 mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ambaye ni Mtendaji wa Kijiji cha Kaulolo amefikishwa mahakamani na kufunguliwa shauri namba 24456/2024.

Ni kwa makosa ya ubadhirifu na ifujaji kinyume na kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Mshtakiwa huyo katika nyakati tofauti alikuwa akikusanya ushuru wa mazao katika Kijiji cha Kaulolo na kutowasilisha fedha benki kiasi cha TZS 15,979,740

Shauri tajwa limesomwa mahakamani na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU,Wakili Vaileth Achimpota mbele ya Mhe. Jackson Ryoba ambaye ni Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Mlele.

Mshtakiwa amekana mashtaka yote na yupo nje kwa dhamana.Kesi hiyo itakuja tena mahakamani Septemba 5,2024 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news