MOROGORO-Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Menejimenti, Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Peter Mwakiluma amehitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko kwa kuwataka kuwa na misingi ya utumishi bora kwa kuvaa mavazi nadhifu sambamba na kufika kazini kwa muda unaotakiwa.Bw. Mwakiluma amesema mtumishi wa umma hupimwa kwa nidhamu yake katika kuwahi kufika ofisini, mavazi anayo yavaa pamoja na kutekeleza majukumu husika.
"Inashangaza kuona mtumishi anachelewa kufika kazini lakini huyo huyo anataka muda wa kutoka atoke muda ule ule sasa jamani tutakuwa hatuwatendei haki wananchi," alisema Bw. Mwakiluma.
Katika mavazi amesisitiza kuwa mtumishi wa umma hutambulika kwa mavazi yake ambayo yapo kwenye msingi wake, akisema mavazi yenye maandishi hayatakiwi sambamba na kuvaa nguo zenye kuonesha sehemu kubwa ya mwili hayatakiwi.