Wazabuni wapewa somo Moduli ya kuwasilisha rufaa

DODOMA-Wazabuni mbalimbali wameendelea kutembelea Banda la Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) na kupatiwa elimu juu ya moduli mpya ya kuwasilisha rufaa/malalamiko kwa njia ya kieletroniki (Complaint & Appeal Management).
Moduli hiyo inarahisisha uwasilishaji wa malalamiko na kutoa fursa kwa wazabuni wengi zaidi kuwasilisha malalamiko yao. Moduli hiyo ni rafiki na inaokoa muda wa kuwasilisha rufaa au malalamiko.

Aidha, Moduli ya Complaint & Appeal Management imewekwa kwenye Mfumo wa Ununuzi wa Umma Kieletroniki (NeST), uliojengwa chini ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

PPAA wanatoa elimu hiyo katika maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nane Nane), yanayoendelea Nzuguni jijini Dodoma kuanzia tarehe 01 – 10 Agosti, 2024. Banda la PPAA liko katika banda kuu la Wizara ya Fedha.

Kauli mbiu ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nane Nane) 2024 ni "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news