Waziri Dkt.Nchemba aongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Africa Caucus Meetings

NA BENNY MWAIPAJA
WF Abuja

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria. Mkutano huo umefunguliwa rasmi tarehe 2 Agosti, 2024 na Makamu wa Rais wa Nigeria, Mhe Kashim Shettima.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Nigeria, Mhe Kashim Shettima (Hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria, ambao unajadili namna ya kuboresha biashara katika nchi za Afrika kwa kuweka mazingira mazuri ya kusisimua biashara kwa kujenga miundombinu itakayowezesha kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika na wataweka msimamo wa pamoja na kupeleka agenda ya namna Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, zinatakiwa kuziwezesha nchi hizo kifedha na kiutaalam ili zifikie malengo husika.
Makamu wa Rais wa Nigeria, Mhe. Kashim Shettima, akifungua Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) ambao Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba, na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango-Zanzibar (hawapo pichani) wameshiriki, unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria, ambao unajadili namna ya kuboresha biashara katika nchi za Afrika kwa kuweka mazingira mazuri ya kusisimua biashara kwa kujenga miundombinu itakayowezesha kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika na wataweka msimamo wa pamoja na kupeleka agenda ya namna Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, zinatakiwa kuziwezesha nchi hizo kifedha na kiutaalam ili zifikie malengo husika.
Baadhi ya Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) pamoja na viongozi wa Benki ya Dunia na IMF, wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 24 (Africa Caucus Meetings) iliyokuwa inatolewa na Makamu wa Rais wa Nigeria, Mhe. Kashim Shettima, katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria, ambapo katika mkutano huo wamejadiliana namna ya kuboresha biashara katika nchi za Afrika kwa kuweka mazingira mazuri ya kusisimua biashara kwa kujenga miundombinu itakayowezesha kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika na wataweka msimamo wa pamoja na kupeleka agenda ya namna Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, zinatakiwa kuziwezesha nchi hizo kifedha na kiutaalam ili zifikie malengo husika.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wa tisa kutoka kulia waliosimama nyuma), akiwa katika picha ya pamoja ya Mawaziri wa Fedha wa nchi za Afrika wakiwa na Mwenyeji wa Mkutano huo ambaye ni Waziri wa Fedha wa Nigeria, Mhe. Wale Edun (wa nane waliosimama mbele kutoka kulia), wakati wa Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria, ambao unajadili namna ya kuboresha biashara katika nchi za Afrika kwa kuweka mazingira mazuri ya kusisimua biashara kwa kujenga miundombinu itakayowezesha kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika na wataweka msimamo wa pamoja na kupeleka agenda ya namna Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, zinatakiwa kuziwezesha nchi hizo kifedha na kiutaalam ili zifikie malengo husika.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Abuja, Nigeria).

Mkutano huo unajadili namna ya kuboresha biashara katika nchi za Afrika kwa kuweka mazingira mazuri ya kusisimua biashara kwa kujenga miundombinu itakayowezesha kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika na wataweka msimamo wa pamoja na kupeleka agenda ya namna Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, zinatakiwa kuziwezesha nchi hizo kifedha na kiutaalam ili zifikie malengo husika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news