Waziri Dkt.Nchemba aweka jiwe la msingi Chuo cha Uhasibu Arusha kampasi ya Babati

MANYARA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameweka jiwe la msingi kwa awamu ya kwanza kati ya awamu tatu za ujenzi wa Kampasi ya Babati ya Chuo cha Uhasibu Arusha na kuupongeza Uongozi wa Chuo hicho kwa ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa mradi huo kwa utaratibu wa force account. Awamu hiyo ya kwanza ya mradi inajumuisha ujenzi wa jengo la taaluma (departmental building), mabweni (hostels) na bwalo la chakula (cafeteria), ambapo ujenzi huo umegharimu shilingi bilioni 10, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 6 zinatokana na mapato ya ndani ya Chuo hicho na kiasi cha shilingi bilioni 4 kimetolewa na Serikali (Wizara ya Fedha), ambayo ni mmiliki wa chuo hicho.
Jengo la taaluma lenye ghorofa tano katika awamu wa kwanza ya mradi huo limefikia asilimia 95 mpaka sasa, likiwa na vyumba vya madarasa, kumbi za mihadhara, vyumba vya Semina, maabara za kompyuta, maktaba, ukumbi wa mikutano na ofisi za wafanyakazi.

Aidha, kwa upande wa mabweni (hostels) yanayojengwa yatakapokamilika yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,456 kwa wakati mmoja na Bwalo la chakula (cafeteria) litakuwa na uwezo wa kuchukua watu 200 kwa wakati mmoja.
Tukio hilo la uwekaji jiwe la msingi limehudhurudhiriwa na viongozi na wadau mbalimbali wa akiwemo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news