Waziri Jafo ahimiza WMA kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa jamii

DODOMA-Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Selemani Jafo (Mb) ametembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika kilele cha Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama Nane Nane jijini Dodoma na kuhimiza kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa wakulima.
Akizungumza na Wataalamu wa WMA wanaoshiriki Maonesho hayo, Mhe. Jafo amepongeza maandalizi mazuri yaliyofanyika na kusisitiza kuwa elimu ya vipimo iendelee kutolewa kwa wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla.
"Elimu ya vipimo ni muhimu sana hivyo hata baada ya Maonesho muendelee kuwaelimisha wananchi," amesema.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kiula, amesema Wakala hiyi itaendelea kutoa elimu ya vipimo kwa wananchi kwa siku mbili zaidi katika Maonesho ya NaneNane kufuatia agizo la Mgeni Rasmi, Rais Samia Suluhu Hassan alilotoa wakati akifunga Maonesho husika yaliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.
Aidha, Kiula ameongeza kuwa WMA itaendelea kutoa elimu kupitia kampeni mbalimbali nchi nzima katika kuhakikisha wananchi wote wanapata uelewa kuhusu matumizi ya vipimo sahihi pamoja na manufaa yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news