Waziri Kombo afanya mazungumzo na Rais wa BADEA

HARARE-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amefanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA), Dkt. Sidi Ould Tah jijini Harare , Zimbabwe tarehe 13 Agosti, 2024.
Mazungumzo yakiendelea.

Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo viongozi hao, wamejadili umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki hiyo ambayo imekuwa ikitoa misaada ya kifedha, mikopo nafuu, na ufadhili kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo barani Afrika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na Rais wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA), Dkt. Sidi Ould Tah walipokutana kwa mazungumzo pembezoni mwa mkutano wa SADC unaoendelea jijini Harare , Zimbabwe tarehe 13 Agosti, 2024.

Aidha, Mhe. Balozi Kombo amemueleza Dkt. Tah kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na wabia wa maendeleo kwa ustawi wa watu wake na Taifa kwa ujumla, hivyo ni matarajio yake kwamba mazungumzo hayo yatafungua maeneo mapya ya ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akisisitiza alipokuwa kwenye mazungumzo na Rais wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA), Dkt. Sidi Ould Tah jijini Harare, Zimbabwe tarehe 13 Agosti, 2024.

Hivyo, katika kuendelea kuimarisha Diplomasia ya Uchumi, Wizara itaendelea kusimamia taratibu za makubaliano ambazo BADEA itaingia na sekta husika ili kuhakikisha nchi yetu inanufaika vyema na fursa za ujenzi wa miundombinu ya kidigitali na upatikanaji wa mawasiliano ya kimtandao (Internet).
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. IGP (RTD) Simon Sirro (kulia) wakifuatilia.

Naye Dkt. Tah ameeleza kuwa Benki hiyo ina nia ya kufadhili nchini Tanzania ujenzi wa Kituo cha kwanza cha kuhifadhi taarifa zinazohusu masuala ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence & Robotics) na kwamba kukamilika kwa taratibu za uanzishwaji wa mradi kutawezesha utekelezaji kuanza kwa wakati. Mazungumzo kuhusu suala hili yanaendelea.
Rais wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA), Dkt. Sidi Ould Tah akiwa kwenye mazungumzo na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo yaliyofanyika jijini Harare, Zimbabwe.
Picha ya pamoja.

Viongozi wengine walioshiriki mazungungumzo hayo ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. IGP (RTD) Simon Sirro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news