Waziri Kombo afanya mazungumzo na mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini na Madagascar

HARARE-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mhe. Ronald Lamola na Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar, Mhe. Dkt. Rasata Rafaravavitafika pembezoni mwa Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) tarehe 14 Agosti, 2024 Harare, Zimbabwe.

Akizungumza na Mhe. Lamola, Waziri Kombo ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano wa kihistoria na kindugu uliopo baina ya Tanzania na Afrika kusini ili kukuza sekta za kiuchumi ikiwemo biashara, utalii, uwekezaji, elimu, afya na maeneo mengine ya kimkakati kwa maslahi ya pande zote mbili.

Naye Mhe. Lamola ameeleza kuwa Afrika Kusini inaendelea kuthamini mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Taifa hilo hivyo, ina nia ya dhati ya kuuenzi mchango huo kwa kukuza ushirikiano katika shughuli za kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa ustawi wa wananchi wa mataifa hayo mawili.

Aidha, katika mazungumzo ya Mhe. Kombo na Mhe. Dkt. Rafaravavitafika wamejadili juu ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi na taifa hilo hususan katika sekta ya uchumi wa blue ambao Tanzania imeuwekea mkazo ili kukuza uchumi kupitia rasilimali za bahari zinazopatikana na kukuza biashara yake kimataifa.

HABARI KATIKA PICHA: Waziri Kombo alipokutana kwa mazungumzo na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mhe. Ronald Lamola.
HABARI KATIKA PICHA: Waziri Kombo alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar, Mhe. Dkt. Rasata Rafaravavitafika

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news