Waziri Kombo ajitambulisha kwa Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), pamoja na Manaibu wake, Mhe. Cosato Chumi (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dennis Londo (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki; wamefanya ziara ya kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu Zanzibar.
Katika utambulisho huo, viongozi hao wamemuhakikishia Rais Mwinyi kuendelea kushirikiana kwa karibu na kuhakikisha kuwa maslahi ya pande zote mbili—Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar—yanapewa kipaumbele. Ziara hii ni hatua muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano kwa manufaa ya wananchi wote wa Tanzania, ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni Wizara ya Muungano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news