Waziri Lukuvi:Rais Dkt.Samia ameagiza kurejeshwa huduma za kijamii Tarafa ya Ngorongoro

ARUSHA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameagiza kurejeshwa kwa huduma za kijamii ikiwemo za elimu na afya zilizokuwa zimesitishwa katika Tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Hayo yamesemwa leo Ijumaa Agosti 23, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi akizungumza na wananchi wa kata 11 zilizopo Tarafa ya Ngorongoro, akiwasilisha maagizo ya Rais aliyewatuma kuwasilikiza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku tano wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Makonda akifuatilia mkutano huo wa Waziri Lukuvi.
Aidha, amesema Rais ameagiza uchaguzi katika tarafa hiyo kwa kutumia mipaka ya zamani, ufanyike kama unavyofanyika maeneo mengine nchini.Tazama video;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news