Waziri Mavunde aitaka sekta binafsi kujiandaa na mapinduzi makubwa ya Sekta ya Madini

DAR-Waziri wa Madini,Mheshimiwa Anthony Mavunde ametoa rai kwa sekta binafsi nchini Tanzania kujiandaa na kuyapokea mageuzi makubwa yanayofanywa kwenye sekta ya madini ili watanzania washiriki kikamilifu kwenye uchumi huu.
Mavunde ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano na kituo cha Televisheni cha Clouds,akielezea mikakati mbalimbali ya Wizara ya Madini.
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza utekelezaji wa sheria na sera za madini kuwezesha kundi kubwa la Watanzania kushiriki na kunufaika na sekta ya madini.

"Tunahimiza viwanda vya ndani kuzalisha bidhaa zenye ubora na shindani zinazohitajika migodini ili kupunguza uagizwaji wa bidhaa nje ya nchi.

"Lengo letu ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma za migodini barani Afrika,tuna eneo la ulipokuwa mgodi wa Buzwagi sasa litagawiwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kuzalisha bidhaa za migodini.
"Kwa sasa baadhi ya wawekezaji wa nje wa viwanda vya kuzalisha bidhaa za migodini wameanza kufungua viwanda Tanzania kwenye eneo hilo la Kahama kwa sharti kwamba lazima waingie ubia na Watanzania.

"Kiasi cha fedha kilichotumika kwa mwaka wa fedha 2022/23 kwenye manunuzi ya bidhaa na huduma ni Trilioni 3.1.
"Hizi ni fedha nyingi sana na lazima zibaki hapa nchini na watanzania kunufaika badala ya kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi.”

Kifungu cha 105 cha Sheria ya Madini Sura ya 123 imetambua rasmi ushiriki wa Watanzania kwenye uchumi wa Madini na hivyo kutoa fursa ya Watanzania wengi kushiriki moja kwa moja kwenye uchumi huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news