Waziri Mhagama akabidhi ofisi kwa Waziri Lukuvi

DODOMA-Waziri wa Afya,Mhe. Jenista Mhagama ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu),Mhe. William Lukuvi katika maeneo ambayo atahitaji kupata taarifa za ziada wakati wa kuratibu shughuli za serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu.
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) ambaye kwa sasa ni Waziri wa Afya,Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akikabidhi Ofisi kwa Waziri wa Nchi katika ofisi hiyo,Mhe. William Lukuvi (wa katikati) na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu katika ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi katika viwanja vya ofisi hiyo jijini Dodoma.

Mhe. Jenista amesema hayo leo Agosti 20, 2024 jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) kwa Mhe. William Lukuvi aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo.

Aidha, Waziri Mhagama amewashukuru watumishi wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), watumishi wa ofisi binafsi ya Waziri Mkuu pamoja na watumishi wa Ofisi binafsi ya Naibu Waziri Mkuu kwa ushirikiano waliotoa wakati alipokuwa katika ofisi hiyo.
Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watumishi, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika hafla ya kumuaga iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watumishi, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika hafla ya kumuaga iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo jijini Dodoma.

“Naomba niwashukuru kwa dhati Watumishi wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Watumishi wa Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu kwa ushirikiano Mkubwa mlionipa, Watumishi wa ofisi hizi wako tayari kufanya kazi kwa moyo na kukupa ushirikiano ili kuhakikisha kwamba malengo yale tuliojiwekea ndani ya Serikali yanatekelezwa.

“Tumefanya kazi usiku na mchana kama ni uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na Mheshimiwa Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ni pamoja na watumishi waliopo kwenye Ofisi hii katika uratibu wa shughuli za serikali,” amebainisha Waziri Mhagama.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akifafanua jambo wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Waziri wa Nchi katika ofisi hiyo ambaye kwa sasa ni Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama na kumpokea Waziri wa Nchi aliyeteuliwa kuongoza Ofisi hiyo Mhe. William Lukuvi katika viwanja vya Ofisi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi akizungumza na baadhi ya watumishi, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo katika Ofisi hiyo mara baada ya kupokelewa katika viwanja vya Ofisi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi akizungumza na baadhi ya watumishi, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo katika Ofisi hiyo mara baada ya kupokelewa katika viwanja vya Ofisi hiyo jijini Dodoma.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi amesema alikabidhi Ofisi hiyo kwa Waziri Mhagama 2014 na kurudi Mwaka 2024 hivyo amekaa nje ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa miaka tisa (9) na kabla alishawahi kuitumikia kama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kwa miaka tisa (9).

“Nimeondoka 2014 na kurudi 2024 na kukabidhiwa Ofisi na Waziri niliyemkabidhi wakati huo ambaye ni Waziri Mhagama, aidha nimefanya kazi kwa karibu na Mhe. Mhagama wakati nikiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, wakati Mhe Mhagama akiwa Katibu wa Chama Bungeni hivyo ni Mapenzi ya Mungu tumekutanishwa tena watu walewale tunaofahamiana, niwahakikishie tutaendelea kushirikiana na Katibu Mkuu na Watumishi wote ili kuhakikisha kwamba tunafanya kazi zetu vizuri,” amesema Waziri Lukuvi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bwa. Anderson Mutatembwa akieleza jambo wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi hiyo ambaye kwa sasa ni Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama na kumpokea Waziri wa Nchi aliyeteuliwa kuongoza Ofisi hiyo Mhe. William Lukuvi katika viwanja vya ofisi hiyo jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (wa pili kulia) akifuatiwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama (wa tatu kulia) akiwa na Katibu Mkuu katika Ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi na (wa kwanza kulia) na Naibu Katibu Mkuu wake Bw. Anderson Mutatembwa wakati wa makabidhiano ya ofisi.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Awali Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi amewapongeza Waziri wa Afya na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kwa kuaminiwa na kuteuliwa kwa nafasi walizopewa.

“Sisi watumishi wenu tunapenda kuwaahidi kwamba tutaendelea kushirikiana nanyi kutekeleza majukumu yetu lakini kuwatumikia wananchi wa Tanzania,” amesema Katibu Mkuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news