Waziri Ridhiwani Kikwete azindua Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana

DODOMA-Serikali imezindua Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 toleo la 2024, ambayo inakwenda kutatua changamoto mbalimbali za vijana nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akibonyeza kitufe katika kompyuta kuashiria uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2007, Toleo la Mwaka 2024 katika maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa iliyofanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center, jijini Dodoma Agosti 12, 2024.

Uzinduzi huo umefanyika Agosti 12, 2024 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akihutubia viongozi, vijana na wadau wa maendeleo ya vijana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa ambalo limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma, Agosti 12, 2024.
Akizungumza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridiwani Kikwete amesema Serikali katika kuhakikisha masuala ya maendeleo ya vijana yanapatiwa mwongozo na mwelekeo imekwisha kamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 na toleo la mwaka 2024.

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema Sera hiyo inaendana na mabadiliko mbalimbali ya jamii, kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi kitabu cha Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana mwaka 2007, toleo la 2024 kwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mary Maganga mara baada ya kuizindua rasmi sera hiyo Agosti, 2024 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi kitabu cha Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana mwaka 2007, toleo la 2024 kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Mark Schreiner baada ya kuzindua sera hiyo Agosti 12, 2024 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi kitabu cha Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana mwaka 2007, toleo la 2024 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule baada ya kuzindua sera hiyo Agosti 12, 2024 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi kitabu cha Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana mwaka 2007, toleo la 2024 kwa Balozi wa Uswis ncjini Tanzania, Mhe. Didier Chasot baada ya kuzindua sera hiyo Agosti 12, 2024 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi kitabu cha Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana mwaka 2007, toleo la 2024 kwa vijana na wadau wa maendeleo ya vijana (juu na chini) baada ya kuzindua sera hiyo Agosti 12, 2024 jijini Dodoma.
"Serikali inaelewa kuwa mchango wa vijana katika maendeleo ya kidijitali ni muhimu sana kwa vile vijana ni wabunifu, wanajua kutumia teknolojia na wanauwezo wa kuleta mabadiliko makubwa katika jamii zetu," amesema Mhe.Ridhiwan

Amesema, ujio wa sera hiyo ya vijana kutachagiza uudwaji wa baraza la taifa la vijana ikiashiria azma ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutatua changamoto zinazo wakabili vijana kwa kuzipatiwa majibu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi kitabu cha Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana mwaka 2007, toleo la 2024 kwa vijana na wadau wa maendeleo ya vijana (juu na chini) baada ya kuzindua sera hiyo Agosti 12, 2024 jijini Dodoma.
Kwa upande mwengine, Waziri Ridhiwani amewataka watendaji wa ofisi yake kuendana na mabadiliko ya sasa katika kuwahudumia wananchi.

Naye, Katibu Mkuu wa ofisi hiyo,Mary Maganga, amesema katika kuadhimisha siku ya vijana, wameendesha kongamano la siku mbili lililokutanisha vijana zaidi ya 3,000 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

"Katika kongamano hilo, vijana wamepata fursa ya kutoa maoni juu ya Dira ya Maendeleo ya 2050, fursa za kidigitali, vijana na uchumi, afya ya akili na saikolojia ya vijana, ajira na uwezeshaji," amesema Maganga.
Naye Mwakilishi wa Vijana, Charles Ruben ametoa pongezi kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuwasaidia na kuwainua vijana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news