Waziri Simbachawene anena ajira mpya kwa walimu na madaktari

DODOMA-“Ninamuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kushirikiana na Katibu Mkuu TAMISEMI ili kuhakikisha shule zote mpya na vituo vya afya nchi nzima vilivyokamilika vinapangiwa Walimu na Madaktari mtawalia”.
Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mhe. George Simbachawene Agosti 7, 2024 wakati alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Wangi Jimbo la Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara alipokuwa akiongea na wananchi na kuzindua Shule ya Sekondari Wangi.
“Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ajira zaidi ya elfu 12 kwa sekta ya afya na nyingine kwa sekta ya elimu, hivyo hatuna budi kuhakikisha wanapangwa vizuri ili wananchi wapate huduma ipasavyo,” alisema Mhe. Simbachawene.
Aidha, Mhe. Simbachawene amewaomba wananchi wa Kata ya Wangi na Wotta kushukuru kwa maendeleo ambayo yameletwa na Rais Dkt. Samia mathalani ujenzi barabara, shule na vituo vya afya kwa lengo la kurahisisha maisha kwa wananchi.
Hivyo, wananchi wameombwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kumpa kura za ndiyo Rais Mhe. Dkt. Samia, Mbunge Mhe. Simbachawene na Madiwani ili waenedelee kutekeleza maono waliyonayo badala ya kuanza upya.
Mhe. Simbachawene anaendelea na ziara yake katika Jimbo la Kibakwe ambapo amefanya mikutano ya hadhara katika Kijiji cha Wotta na Wangi Jimbo la Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news