Waziri Soraga azindua Tamasha la Mswahili wa Pemba

ZANZIBAR-Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga hivi karibuni amezindua Tamasha la Mswahili wa Pemba lilofanyika Mkoa wa Kaskazini Pemba.Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa tamasha hilo, Mhe. Mudrik amesema kwamba,amefurahishwa na Utamaduni wa Wananchi wa Kojani pamoja na mashirikiano yao katika kufanikisha tamasha hilo kuanzia utayari, na kujitokeza kwa wingi katika kuunga mkono tamasha hilo.
Mhe. Soraga ameeleza kuwa, Tamasha la Mswahili wa Pemba ni tamasha ambalo lina ishara zote za kuifungua Pemba katika masuala ya utalii kwa kuwa limewavutia zaidi wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo.

Vilevile tamasha hilo limeweza kutoa fursa kwa wageni kujifunza vyakula vya asili, mila,silka na utamaduni za watu wa Pemba.

Tamasha hilo limehusisha michezo mbalimbali ya baharini ikiwemo resi za Ngalawa kwa upande wa Wanawake na Wanaume, Ngoma za Asili,Mchezo wa Ngumi, kuvuta kamba na mengine mengi.

Akitoa wito katika tamasha hilo,Mhe. Soraga amewaomba na kuwataka wananchi wa Kojani kuendelea kudumisha mila na desturi pamoja na tamaduni zao kwani zimeonekana kua kivutio kwa wengi walioshiriki Tamasha hilo.
Naye Afisa Mdhamini Afisi Kuu Pemba, Zuhura Othman amesema kuwa, Tamasha la Mswahili wa Pemba linalenga kuunga mkono Dira na Maono ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kuutangaza Utalii wa Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news