Dkt.Nchemba apigia chapuo uwekezaji mitaji kutoka nje na lugha ya Kiswahili nchini Nigeria

NA BENNY MWAIPAJA
WF Abuja

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa na Ujumbe wa Tanzania katika Ubalozi wa Tanzania, uliopo Abuja nchini Nigeria, ambapo yeye na ujumbe wake, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango-Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, wanashiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), ukiwashirikisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), akiteta jambo na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Bi. Judica Nagunwa, baada ya kufika katika ofisi za ubalozi wa Tanzania uliopo Abuja nchini Nigeria, ambapo anashiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), unaowashirikisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Mhe. Dkt. Nchemba na ujumbe wake walipowasili katika Ubalozi huo, walilakiwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Bi. Judica Nagunwa akiambatana na Mwambata Jeshi wa Ubalozi Brigedia Jenerali Julius Kadawi na Maafisa wengine waandamizi.

Akizungumza na Watumishi wa Ubalozi, Mhe. Dkt. Nchemba, aliupongeza Ubalozi huo kwa kusimamia vema Diplomasia ya kiuchumi na kuvutia uwekezaji na mitaji kutoka katika Taifa hilo kubwa barani Afrika.
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza jambo wakati wa kikao kifupi alipotembelea ofisi za ubalozi wa Tanzania uliopo Abuja nchini Nigeria, ambapo anashiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), unaowashirikisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Alitoa wito kwa Ubalozi huo kufanya utafiti namna lugha ya kiswahili inaweza kunadiwa katika Mataifa kadhaa ya kiafrika wanayoyasimamia kutokana na umuhimu wa lugha hiyo katika kuunganisha Bara hilo.

Alisema kuwa, kiswahili ni bidhaa ambayo ikienea na kutumiwa na Mataifa mengi duniani itakuza ajira kwa walimu wa kitanzania watakaotumika kufundisha lugha hiyo lakini pia kuharakisha maendeleo katika nchi zitakazozungumza lugha hiyo.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Bi. Judica Nagunwa (Kulia) akiwakaribisha Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa kwanza alieketi), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa pili alieketi) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango-Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi (wa tatu alieketi), wakati walipofika katika ofisi za ubalozi wa Tanzania uliopo Abuja nchini Nigeria, ambapo wanashiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), unaowashirikisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Bi. Judica Nagunwa, alisema watalifanyia kazi suala la kukuza matumizi ya kiswahili katika nchi wanazoiwakilisha nchi na kwamba tayari kuna Ushirikiano na makubaliano ya kitaasisi kati ya Tanzania na Nigeria katika kueneza lugha ya kiswahili kupitia vyuo vikuu vya Tanzania na Nigeria lakini pia kupitia Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa pili kushoto), Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Bi. Judica Nagunwa (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa kwanza kulia) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango-Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi (wa kwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelea ubalozi wa Tanzania uliopo Abuja nchini Nigeria, ambapo wapo nchini humo kushiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), ukiwashirikisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Aidha, Bi. Nagunwa alisema kuwa Nigeria ni nchi kubwa kiuchumi na kwamba Tanzania imenufaika na uwekezaji wake nchini Tanzania, kikiwemo Kiwanda cha Saruji cha Dangote na Benki ya UBA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news