ZANZIBAR-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. Adolf Mkenda amesema, wizara inatekeleza miradi na kutoa mikopo na ufadhili wa Samia Skolashipu kwa wanafunzi katika vyuo vyote vya Elimu ya Juu ikiwemo Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume (KIST).
Akizungumza katika sherehe za Miaka 50 ya Idara ya Ujenzi ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia Karume (KIST),
Prof. Mkenda amesema kupitia ufadhili wa Serikali ya Italia Wizara inatekeleza mradi wa Tanzania Education Labour Market Support ambao umetoa fedha kwa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume (KIST), Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT), Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Chuo vha Ufundi Arusha (ATC).
Mradi huo mradi wa miaka mitano unalenga kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia sambamba na kuboresha programu za mafunzo ya ufundi katika uhifadhi wa mazingira na nishati endelevu.
Ameipongeza Taasisi ya KIST kwa mafanikio mbalimbali tangu kuanzishwa kwake Mwaka 1973.