Wizara tatu zajadili hali ya uzalishaji chumvi nchini

DODOMA-Wizara za Madini, Mipango na Uwekezaji ikiwemo Viwanda na Biashara zimekutana kujadili namna ya kuondoa changamoto katika sekta ndogo ya chumvi nchini.
Wizara hizo zimekutana leo Agosti 15 , 2024 jijini Dodoma kufuatia taarifa zilizowasilishwa kwa Serikali na Chama cha Wazalishaji Chumvi Tanzania (TASPA) kuhusu changamoto zinazoikabili sekta hiyo ndogo ya chumvi ikiwemo kudorora kwa biashara ya chumvi hapa nchini.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Madini,Mhe.Anthony Mavunde amesema kuwa, takwimu za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Tume ya Madini zinaonesha makadirio ya chumvi inayotumika nchini ikijumuisha chumvi ya viwandani na mezani ni wastani wa tani 324,279 kwa mwaka.
Aidha, Waziri Mavunde amefafanua kuwa kiwanda cha kampuni ya Neelkanth kwa sasa kina hitaji kiasi cha tani 14,000 kwa mwezi za chumvi ghafi sawa na takribani tani 168,000 kwa mwaka.
Kwa mujibu wa tathmini ndogo iliyofanywa na Tume ya Madini kwa kushirikiana TASPA imeonesha uwepo wa takribani tani 56,286 ambapo tani 50,000 mkoani Tanga, tani 6056 Kigoma na tani 230 mkoani Mtwara.

Kikao hicho kilijumuisha mawaziri wa wizara zote tatu pamoja na watendaji mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news