Wizara ya Fedha yatoa maelekezo kwa taasisi za Serikali kuhusu mikopo

SCOLA MALINGA NA
JOSEPH MAHUMI

WIZARA ya Fedha imezitaka taasisi za Serikali kuhakikisha kuwa zinafuata Sheria na Miongozo ya ukopaji fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na taasisi hizo.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama, akifungua magunzo na Elimu kwa Taasisi za Serikali, kuhusu matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, kwa Niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa itawajengea uwezo taasisi hizo ili kifuata sheria hiyo inauompa mamlaka Waziri wa Fedha kusimamia mikopo, dhamana na misaada ambayo nchi inapata kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kutekelezaji miradi ya maendeleo.

Rai hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Wizara ya Fedha, Bwana Omary Khama, wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kwa Taasisi za Serikali kuhusu matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada namba 134 pamoja na miongozo mbalimbali katika kufadhili miradi ya maendeleo.
Mchumi kutoka Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Abeid Mzee, akiwasilisha mada inayohusu mambo ya kuzingatia wakati wa kuandaa maandiko ya miradi, wakati wa mafunzo na Kutoa Elimu kwa Taasisi za Serikali, kuhusu matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa hatua hiyo inachukuliwa ili kuhakikisha kuwa matakwa ya Sheria hiyo inayoelekeza kuwa mwenye dhamana ya kukopa kuweka dhamana na kupokea misaada ni Waziri wa Fedha.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, akizungumza jambo wakati wa utoaji Elimu kwa Taasisi za Serikali, kuhusu matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, iliyofakatika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa ni lazima Taasisi ziandae maandiko ya miradi ikihusisha uoembuzi yakinifu, kuwa na timu mahili za kusimamia miradi pamoja na Wizara husika kutenga bajeti ya kutekeleza miradi husika kwa ufanisi.
Baadhi ya Washiriki kutoka Taasisi za Serikali wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kuhusu elimu ya matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Bw. Khama alisema kuwa Sheria namba 134 ya Mikopo, Dhamana na Misaada, imelenga kuhakikisha kuwa Serikali inakopa mikopo yenye gharama nafuu pamoja na kuepuka masharti hası ya mikopo husika.

Wizara ya Fedha inatoa mafunzo kuhusu vipengele mbalimbali vya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na taratibu na mazingatio yanayohusiana na Sheria ya mikopo, dhamana na misaada Sura ya 134, pamoja na mwongozo wa utambuzi wa miradi, uandaaji, utekelezaji, na majadiliano ya mikopo na misaada kwa ajili ya kufadhili miradi ya maendeleo.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja kutoka Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga UWASA), Bw. Alawi Ahmadi, akichangia jambo wakati wa mafunzo ilioandaliwa na Wizara ya Fedha kuhusu elimu ya matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam).

“Mwongozo una lengo la kusaidia maendeleo ya masoko ya kifedha ya ndani na nje na kuhakikisha kuwa madeni yasiyo ya lazima yanaepukwa.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news