Wizara ya Fedha yazitaka mamlaka za Serikali za mitaa na sekta binafsi kutumia fursa zilizopo katika Sheria ya PPP

PETER HAULE NA
JOSEPH MAHUMI

WAZIRI wa Fedha,Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ametoa rai kwa mamlaka za Serikali pamoja na wawekezaji kutoka sekta binafsi kutumia fursa zilizopo katika Sheria ya Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPP) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ili kupata faida na kuipunguzia Serikali mzigo wa kibajeti.
Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kushoto walioketi), Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wapili kushoto walioketi), Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Dkt. Festo Dugange (Katikati), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Mikoa baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma.

Mhe. Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, sura Na. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi, Sura Na. 103.
Sambamba na mafunzo ya matumizi ya takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma, uliopo Mji wa Serikali Mtumba.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati akifungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa
na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma, ambapo amewasihi viongozi hao kutumia vyema mafunzo hayo katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika ununuzi wa vifaa na utekelezaji wa miradi kupitia Mfumo wa Ununuzi wa umma (Nest) na fursa ya kutekeleza miradi kwa njia ya Ubia.

Amewahimiza Maafisa Masuuli wote kuzingatia maelekezo ya Waraka wa Hazina namba 7 wa mwaka 2020/21 unaotoa maelekezo na mwongozo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa utaratibu wa PPP.

Amesema kuwa,Sheria ya PPP Sura 103 imefanyiwa marekebisho kwa kuweka mazingira wezeshi ili kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, Sheria hiyo inaruhusu wawekezaji katika miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kunufaika na vivutio vya kikodi na visivyokuwa vya kikodi, sawa na wale wanaopata vivutio chini ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania, Sura ya 38.

“Sheria ya PPP inaruhusu taasisi za umma kununua mbia anayekidhi vigezo moja kwa moja kwa miradi isiyohitaji ushindani ili kupunguza muda wa hatua za ununuzi na pia imetoa fursa kwa wawekezaji wa kigeni kushirikisha wazawa katika miradi ya PPP ili kuwawezesha kiuchumi na kuendeleza wataalamu wa ndani,”amesema Dkt. Nchemba.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kufungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma, ambapo amewasihi viongozi hao kutumia vyema mafunzo hayo katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika ununuzi wa vifaa na utekelezaji wa miradi kupitia Mfumo wa Ununuzi wa umma (Nest) na fursa ya kutekeleza miradi kwa njia ya Ubia.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi, Jenifa Christian Omolo, akizungumza wakati wa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, akizungumza wakati akizungumza wakati akitoa neno la shukrani kabla ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma, ambapo amewasihi viongozi hao kutumia vyema mafunzo hayo katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika ununuzi wa vifaa na utekelezaji wa miradi kupitia Mfumo wa Ununuzi wa umma (Nest) na fursa ya kutekeleza miradi kwa njia ya Ubia.

Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma, ambapo amewasihi viongozi hao kutumia vyema mafunzo hayo katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika ununuzi wa vifaa na utekelezaji wa miradi kupitia Mfumo wa Ununuzi wa umma (Nest) na fursa ya kutekeleza miradi kwa njia ya Ubia.

 Akizungumzia suala la matumizi sahihi ya Takwimu Dkt. Nchemba alisema kuwa maendeleo ya Taifa lolote ulimwenguni yanatokana na matumizi sahihi ya takwimu zilizozalishwa na vyombo vyenye jukumu hilo katika kupanga mikakati mbalimbali ya maendeleo.

Alisema kuwa utekelezwaji wa mipango yote ya mendeleo nchini Tanzania umekuwa ukifanywa kwa kuzingatia takwimu zilizoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambayo ilianzishwa kwa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 ambayo imeipa mamlaka ya kuandaa na kuchapisha takwimu mbalimbali zinazohitajika kwa matumizi ya kimaendeleo ikiwemo kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Dkt. Nchemba alisema pamoja na kuwepo kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu inayofanya kazi nzuri ya kutoa takwimu mbalimbali, bado matumizi ya takwimu hizo katika upangaji na utekelezaji wa mipango hauridhishi, kwa kuwa mara kadhaa imetiliwa mashaka kama ilitumia takwimu sahihi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

“Mipango yenye mashaka inatupotezea muda lakini pia imekuwa ni chanzo cha kutofanikishwa kwa malengo mbalimbali hususani malengo ya kutoa huduma bora kwa wananchi, natoa rai kwa taasisi zote za umma hapa nchini kuhakikisha zinazingatia na kuongeza matumizi ya takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kuandaa mipango yote muhimu kwa kadri inavyowezekana,”amesisitiza Dkt. Nchemba.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange, alisema kuwa katika historia ya nchi ya Tanzania hakuna kipindi ambacho Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa zimetekeleza miradi mingi kama kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema, bajeti kubwa ya Serikali inaenda TAMISEMI na kwa kiasi kikubwa inatumika kwenye ununuzi katika utekelezaji wa miradi lakini pia shughili mbalimbali za kiofisi.
Alisema kuwa katika taarifa nyingi za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kumekuwa na changamoto kubwa kwenye eneo la ununuzi, hivyo mafunzo hayo ni fursa muhimu kwa watendaji walioshiriki ili kuweza kutekeleza shughuli zao hususani za ununuzi lakini kutumia takwimu sahihi kupanga mipango ya maendeleo
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma, ambapo amewasihi viongozi hao kutumia vyema mafunzo hayo katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika ununuzi wa vifaa na utekelezaji wa miradi kupitia Mfumo wa Ununuzi wa umma (Nest) na fursa ya kutekeleza miradi kwa njia ya Ubia.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma, ambapo amewasihi viongozi hao kutumia vyema mafunzo hayo katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika ununuzi wa vifaa na utekelezaji wa miradi kupitia Mfumo wa Ununuzi wa umma (Nest) na fursa ya kutekeleza miradi kwa njia ya Ubia.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma, ambapo amewasihi viongozi hao kutumia vyema mafunzo hayo katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika ununuzi wa vifaa na utekelezaji wa miradi kupitia Mfumo wa Ununuzi wa umma (Nest) na fursa ya kutekeleza miradi kwa njia ya Ubia.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma, ambapo amewasihi viongozi hao kutumia vyema mafunzo hayo katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika ununuzi wa vifaa na utekelezaji wa miradi kupitia Mfumo wa Ununuzi wa umma (Nest) na fursa ya kutekeleza miradi kwa njia ya Ubia.

Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa walioshiriki Mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Bw. Martin Shigella, alisema kuwa wanapopata majukwaa ya mafunzo kama hayo yanasaidia kujua jambo gani la kufanya ili kusukuma jambo ambalo limekwama katika mkoa husika.

Aidha alimshukuru Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Nchemba kwa kuwaalika na wapo tayari kufanyia kazi yale yote yatakayowasilishwa kupitia mada mbalimbali katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

Mkutano huo umewashirikisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news