Yaliyojiri banda la Wizara ya Fedha maonesho ya Nanenane jijini Dodoma


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (katikati mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara hiyo, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Thobias Makoba (wapili kushoto), akifurahia maelezo kutoka kwa Mchumi Mkuu Kutoka Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Bi. Salome Kingdom (kulia), kuhusu umuhimu wa Sera ya fedha katika maendeleo ya wananchi, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”. Wa kwanza Kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhan Kissimba.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Binafsi (PPP Centre), Bw. David Kafulila (wa pili kushoto), kuhusu majukumu ya Kituo hicho, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Afisa Tehama Mwandamizi, Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Zaina Mwanga (katikati), akimwelekeza Mkazi wa jiji la Dodoma, Bw. Ernest Aloyce (kulia), namna ya kufanya malipo ya Huduma za Serikali kupitia Application ya GePG, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”. Kushoto ni Afisa Usimamizi wa Mifumo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Emmanuel Maendaenda.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Binafsi (PPP Centre), Bw. David Kafulila (kushoto), akisikiliza kwa umakini maelezo ya Afisa Hesabu kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bi. Mercelina Haule (kulia), kuhusu, majukumu ya Huduma ya Mfuko Mkuu, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”. Katikati ni Mhasibu Mkuu kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA (T), Denis Luzari.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (kulia), akifurahia jambo na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini - GPSA, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo (kushoto), akiwaeleza wakazi wa Dodoma kuhusu namna ya kujipanga na kustaafu, wakati walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Fedha).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news