Young Africans Sports Club walipaswa kupata mabao zaidi ya 7-Msigwa

NA DIRAMAKINI

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Gerson Msigwa amesema Young Africans Sports Club ilipaswa kupata ushindi wa mabao zaidi ya saba dhidi ya Vital'O FC ya Burundi.
"Yanga walikuwa wanaweza kupata zaidi ya mabao saba leo, lakini wamepata hayo manne, ni jambo la heri, siyo mbaya tumeanza kwa pointi tatu na magoli manne ni kitu kizuri."

Hayo yamejiri baada ya Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Young Africans Sports Club ya jijini Dar es Salaam kuwachapa Vital’O mabao hayo katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.


Mtanange huo umepigwa Agosti 17,2024 katika dimba la Chamazi Complex lililopo Kata ya Chamazi ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar Es Salaam.

Msigwa ameyasema hayo baada ya kukabidhi shilingi milioni 20 kwa uongozi wa Yanga SC ikiwa ni sehemu ya fedha za hamasa ya ushindi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.


Aidha, amesema ni matarajio ya Watanzania na Taifa kwa ujumla kuona klabu zote zinazoshiriki michuano ya Kimataifa zinafanya vizuri ikiwemo timu ya Taifa.

Wawili hao wanatarajiwa kurudiana Agosti 24, mwaka huu ambapo mechi itachezwa hapa hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news