ZANZIBAR-Zanzibar inaendelea kushika kasi katika mbio za kuongoza safari nyingi za ndege katika mataifa ya Afrika Mashariki ambapo imefikia jumla safari 75 kwa siku nyuma ya Mataifa mawili Ethiopia pamoja na Kenya.
Kwa mujibu wa tovuti ya 'Flight from' imetaja takwimu hizo ya kwamba Kiwanja cha ndege Ethiopia ndiyo kimeongoza kwa kuwa na safari nyingi kwa jumla ya safari 186 huku Uwanja wa NBO Nairobi ukishika nafasi ya pili wenye jumla ya Safari 123 ikifuatiwa na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume Zanzibar wenye jumla ya safari 75
Aidha, takwimu hizo pia zimeitaja kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amaan Karume Zanzibar kuingia katika kumi bora ya Viwanja vya ndege vyenye safari nyingi kwa siku Afrika nzima zipatazo 75.