ZFF yatoa ufafanuzi kuhusu New Amaan Complex

ZANZIBAR-"Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) linapenda kuwatoa hofu wadau na wapenzi wa mpira wa miguu nchini na kupuuza taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Uwanja wa New Amaan Complex haujaruhusiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) kutumika katika mzunguko wa pili (2nd preliminary round) ya mashindano ya vilabu bingwa Afrika.

"Aidha, ZFF inapenda kuwataarifu umma kuwa, Uwanja wa New Amaan Complex umepitishwa na CAF kutumika katika Mzunguko wa Awali na pili, hivyo bado ruhusa ya Uwanja wa Amaan Complex kutoka CAF ipo pale pale, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya CAF iliyotolewa tarehe 27 Julai 2024 na tarehe 26 Agosti 2024."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news