Zuchu aahidi kumnunulia msanii mwenzake Angellah gari leo

NA DIRAMAKINI

MSANII wa kizazi kipya Tanzania kutoka Lebo ya WCB, Zuhura Othman Soud (Zuchu) ameahidi kumnunulia msanii mwezake wa Bongo Fleva,Angelina Samson (Anjella) gari.
Zuchu ametoa ahadi hiyo usiku wa Agosti 21,2024 katika kipindi cha Lavi Davi ambacho huwa kinarushwa na Wasafi FM kuanzia saa 4 usiku hadi 6 kila siku.

Uamuzi huo umekuja baada ya Angella kumpigia simu Zuchu na kumweleza kuwa atafarijika kama atapata msaada wa gari,kwani mara nyingi amekuwa akitumia Bolt kwenda kwenye shughuli zake.

Hata hivyo, usafiri huo licha ya kumgharimu kutoka Mbweni kuja mjini analazimika kutumia gharama kubwa.

"Hilo limeisha dada yangu, kesho mpange muda tu utapata," Zuchu ameahidi akiwa nyumbani na mume wake Diamond.

Kwa upande wake, Angellah mbali na kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kufika katika kipindi hicho japo kwa kuchelewa amemshukuru Zuchu na Diamond kwa moyo wao wa upendo.

Angellah katika kipindi hicho ambacho kilikuwa kinaongozwa na Diva The Bawse alisikika akitoa machozi ya furaha kwa ahadi hiyo ambayo itatimizwa Agosti 22,2024 jijini Dar es Salaam.

Vile vile, Angellah amemshukuru Diva The Bawse kwa kufanya naye mahojiano ambayo yamewezesha kupata zawadi ya gari kutoka kwa Zuchu.

Baada ya kusainiwa na Wasafi, Zuchu amewapiku weledi waliomtangulia na kuwa kipenzi cha wengi hasa mashabiki wa muziki wa Bongofleva ulio na mvuto zaidi kwa vijana ndani na nje ya Tanzania.

Pia, Zuchu anashikilia rekodi ya msanii wa kike Afrika Mashariki mwenye wafuasi wengi huku akitajwa kuwa na upendo na sapoti kwa wasanii mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news