Afisa Mtendaji matatani kwa ubadhirifu Mbeya

MBEYA-Mahakama ya Wilaya ya Kyela mkoani hapa imemuhukumu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kisyosyo,Anania Agripa Mwalukanga, kulipa faini ya shiligi 500,000 au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la ubadhirifu.
Kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329.

Hukumu dhidi ya Mwalukanga katika shauri la jinai Na. 21763/2024 ilitolewa Agosti 30, 2024 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kyela, Paul Mabula.

Aidha,kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Bw. Sospeter Tyeah.

Ilielezwa kuwa,mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani kwa shtaka la ubadhirifu wa fedha mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyela aliyekuwa na jukumu la kukusanya fedha za ushuru wa halmashauri.

Mshtakiwa alikusanya shilingi 1,897,459 kwa kutumia mashine ya POS ambapo hakuziwasilisha halmashauri na badala yake alizitumia kwa manufaa yake binafsi.

Mahakama iliamuru mshtakiwa kurejesha fedha shiligi 1,897,459 alizozitumia kwa manufaa yake ambazo alizirejesha sambamba na kulipa faini ya shilingi 500,000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news