Akiba Commercial Bank Plc (ACB) yazindua Kampeni ya Tupo Mtaani Kwako

DAR-Taasisi za kifedha hazina budi kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi kwa kuwasogezea karibu ili kusaidia kupunguza adha ya kutumia muda mwingi kufuata huduma umbali mrefu na kuchelewa kufanya shughuli zao za kiuchumi.
Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Akiba Commercial Bank Plc, Bw.Danford Muyango akizindua rasmi kampeni ya Tupo Mtaani Kwako katika tawi la Kijitonyama, Letsya Tower jijini Dar es Salaam.

Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo Biashara cha Akiba Commercial Bank Plc (ACB), Danford Muyango ameyasema hayo Septemba 20,2024 wakati akizindua rasmi Kampeni ya Tupo Mtaani Kwako katika tawi la Kijitonyama la benki hiyo la Letsya Tower.

Amesema,wapo mtaani kila mahali wakitoa huduma ikiwemo elimu ya mikopo, jinsi ya kutumia huduma za kidigitali, VISA card,ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking.
Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Akiba Commercial Bank Plc, Bw.Danford Muyango akizindua rasmi kampeni ya Tupo Mtaani Kwako katika tawi la Kijitonyama, Letsya Tower jijini Dar es Salaam.

"Tumezindua rasmi programu yetu ya TUPO MTAANI KWAKO kupitia timu yetu bobezi ya mauzo sasa tunakufikia popote ulipo nchi nzima kupitia timu yetu ya mauzo kupata huduma zetu za kufungua akaunti, elimu ya mikopo pamoja na jinsi ya kutumia huduma zetu za kidijitali za VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking,"amesema Afisa Biashara huyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Akiba Commercial Bank Plc walioshirika katika uzinduzi wa programu ya Tupo Mtaani Kwako.

Muyango amesema, programu hiyo inaenda sambamba na Kampeni ya Road Show ya kutoa utambulisho kwa timu ya Tupo Mtaani Kwako katika vitongoji na mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news